MAHAKAMA YAMHUKUMU WEMA SEPETU KWENDA JELA MIEZI MITATU

Ile kesi ya kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni Meneja wa Hoteli ya Mediteranian iliyopo Kawe Beach, Dar, Godlucky Kayombo iliyokuwa ikimkabili Wema Sepetu imetolewa hukumu yake baada ya Wema kuomba iharakishwe kwakuwa alikuwa anasafari.

Kwa mujibu wa mtandao wa Global Publishers, Wema Sepetu amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu gerezani ama faini ya shilingi laki moja kwa maana ya elfu hamsini kwa kila kosa baada ya kukutwa na hatia ya kutenda makosa hayo mawili ya kupiga na kutukana.

Baada ya kusomewa hukumu hiyo Wema alitoa laki moja hiyo iliyokuwa ikihitajiwa na mahakama kabla ya kuachiwa huru kuendelea na mishe zake nyingine


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo