Basi la Kampuni ya Hood Limited lenye namba za usajili T 159 AXM
lililokuwa linatoka Mbeya kuelekea Arusha limepinduka katika eneo la
Melela- Mlandizi, Mvomero mkoani Morogoro mchana wa leo na kuua mtu
mmoja huku likiwaacha majeruhi kadhaa.
Imeelezwa kuwa basi hilo lilipinduka wakati dereva akilikwepa lori lililokuwa likijaribu kulipita gari jingine kwenye kona: ‘Mimi nilikuwa natoka Mbeya naenda Moshi kwa ajli ya sikukuu ya Krismas, dereva wetu amefanya kazi kubwa sana ya kuokoa maisha yetu.

Tulipofika
hapa kwenye kona, dereva wetu baada ya kuona lori limejaa upande wetu
akaamua kukwepa kugongana nalo uso kwa uso na kuingia huku lilipo.
Binafsi nampa pongezi nyingi dereva wa hili basi letu,” abiria Bi. Ruth
Mwambogoso amenukuliwa na GPL akisema hayo.
Picha zifuatazo ni kwa hisani ya Dunstan Shekidele wa GPL.
Picha zifuatazo ni kwa hisani ya Dunstan Shekidele wa GPL.