Mkali
wa bongo fleva Abelnego Damian 'Belle 9' Aliwahi kukumbwa na zahma
mbaya ya kufumaniwa chumbani na mke wa mtu jambo ambalo lilimalizwa kwa
kuminywa chini kwa chini lakini habari hiyo haikubumburuka wala
kulipotiwa mahali popote.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho pia ni msanii mkubwa katika game la muziki (jina lipo kwenye droo zetu) Bele alipata kashfa hiyo mwaka 2010 ambapo siku ya tukio alikuwa chumbani kwake na mwanamke huyo ambaye hakujua kama ni "mali ya mtu"
Aidha
"mtonyaji" wetu alizidi kuweka bayana kuwa, bahati nzuri Belle 9
alikuwa anafahamiana vyema na mfumaniaji huyo ambapo alikuwa muungwana
kwa kuomba msamaha huku akiipoza ishu hiyo kwa misimbazi kadhaa "ishu
haikuwa ya kitoto . Waliyamaliza chumbani humo humo lakini Belle 9
alivunja kabisa uhusiano wa aina yeyote na mwanamke huyo.Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho pia ni msanii mkubwa katika game la muziki (jina lipo kwenye droo zetu) Bele alipata kashfa hiyo mwaka 2010 ambapo siku ya tukio alikuwa chumbani kwake na mwanamke huyo ambaye hakujua kama ni "mali ya mtu"
Mdakuzi wetu alipomtafuta Belle 9 kwa njia ya simu , alikiri kukumbwa na jambo hilo huku akisisitiza kulisahau. "Duh! hiyo ni kitambo sana ujue, ila anyway ni kweli lakini halikuwa fumanizi kama unavyosema, wala hakuwa mke wa mtu zaidi ya mapenzi ya kawaida" alisema Belle 9
