WIZARA YA ELIMU YAZIDI KUBANWA BUNGENI KUHUSU "DIVISION" SIFURI

Naibu spika Job Ndugai asubuhi hii ameitaka serikali kuharakisha kuleta taarifa kamili bungeni endapo daraja sifuri limefutwa na kuwekwa daraja la tano badala ya sifuri ama la

Mh Ndugai ametoa kauli hiyo kufuatia mbunge wa Kawe mh. Halima Mdee kuomba muongozo wa spika kufuatia kauli za kukanganya zinazotolewa na viongozi wa wizara ya elimu

Ndugai amesema ni vyema serikali ikatoa taarifa ya ufafanuzi wa suala hilo haraka iwezekanavyo kwa kuwa wanafunzi wa kidato cha nne wanaendelea na mitihani ya kidato cha nne sasa, hivyo si vizuri wanafunzi hao wakaendelea kufanya mitihani ilihali hawajui mpangilio wa madaraja ukoje kwa kuwa kila mtu anatoa taarifa yake

Waziri wa sera, uratibu na bunge William Lukuvi amelihakikishia bunge kuwa serikali itatoa taarifa hiyo mapema ambayo anaimani itatoa mkanganyiko huo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo