Kamanda Kova jana akizungumza na wanahabari amesema Polisi wa jijini Dar es Salaam wamelikamata gari aina ya
Noah lenye namba za usajili T 437 CCJ, lenye rangi nyeusi, ambalo
linatuhumiwa kuhusika katika uporaji wa mikoba.
Gari hilo lilikamatwa Oktoba 29, 2013 majira ya saa 2 usiku huko maeneo ya Kijitonyama na ndani yake mlikutwa mikoba mitatu ya kike, begi jeusi lenye nguo za kiume na Shilingi 700,000 taslimu.
Begi hilo, mali ya Pius Philipo liliibwa kutoka kwenye gari aina ya Toyota Harrier baada ya kuvunjwa kioo na baada ya muda

walijitokeza vijana wawili, ambao ni
Mbarouk Said (30) na Sultan Masoud (28), wote wakazi wa Ilala wakidai
kwamba gari hilo ni lao na kudai walimkodishia gari hilo Udenda.
Baada ya ufuatiliaji, walimkamata mtuhumiwa Abdulraufu Hussein (18), mkazi wa Buguruni Mlapa ambaye alipopekuliwa alikutwa na simu mbili za mkononi aina Samsung Galaxy, mifuko tisa ya kuhifadhia laptop, hati mbili za kusafiria, tai tisa zenye nembo ya Tanapa, kadi mbili za benki, noti mbalimbali za kichina na nyaraka za watu mbalimbali.
Alisema awali gari hilo lilikuwa limeegeshwa nyuma ya gari lenye namba za usajili T 186 BKL aina ya Toyota Harrier, mali ya Pius, ambapo ndipo walipoiba begi jeusi lililokuwa na fedha.
--- taarifa via gazeti la HabariLeo.