POLISI YAWAKAMATA WATUHUMIWA WALIOMJERUHI DK. SENGONDO MVUNGI

PIX 1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba. Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kulia ni Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova. 
PIX 2
PIX 3
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akiwaonyesha waandishi wa habari mapanga waliyoyakamata wakati wa msako mkali wa kuwasaka watuhumiwa waliomvamia na kumshambulia Dk Sengondo Mvungi Mjumbe wa Tume ya Katiba. Katika msakao huo watuhumiwa tisa walikamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi. Katikati (waliokaa meza kuu) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. 
PIX 4
Sehemu ya waandishi habari waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alipokuwa anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari vya nchini na nje ya nchi kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba. Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. 
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
========
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam linawashikilia watu tisa kwa tuhuma za kumvamia na kumjeruhi vibaya Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dk.Sengondo Mvungi hivi karibuni.

Mkasa huo ulimkumba Dk.Mvungi usiku wa kumakia November 3 mwaka huu akiwa nyumbani kwake Mpigi Magoe nje kidogo ya jiji la Dar Es Salaam.

Ni waziri wa mambo ya ndani akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuhusiana na tukio hilo.
 
Watuhumiwa wanaoshikiliwa ni pamoja na Msingwa Mpolela, Chibango Magozi, Ahmed Ally maarufu kama Khatibu, Zacharia Raphael Msesa mwendesha bodaboda, Manda Saluwaa, Paulo Jailof maarufu kama Donondo, Juma Hamis Kangawaa na Mondishu Semaliki wote wakazi wa Dar es Salaam.

Juhudi hizi za kuwatafuta wahalifu, zikazua maswali kuhusiana na ukimya wa jeshi hilo kushindwa kuwapata watekaji na watesaji wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absolum Kibanda na aliyekuwa kiongozi wa madaktari Dr Stephen Ulimboka ambao hadi sasa hawajakamatwa.

Kwa sasa Dk.Mvungi anaendelea na matibabu katika hospitali ya Milpark Johannesburg nchini Afrika Kusini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo