Mwanaume
wa China ameshinda kesi ya kulipwa $120 000 ( tsh.192, 840,000/=) baada
ya kumpa taraka mke wake kwa kumzalia watoto wabaya.
Awali,
mwanaume huyo aitwaye Jian Feng, alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa
anatoka nje ya ndoa kwakuwa haikuwa ikimuingia akilini kuzaa watoto
wasiovutia kama wao..
Baada ya DNA kuweka bayana kuwa kweli watoto ni wa kwake, mke wa Feng aliamua kuitoa siri nyingine ndogo.
Kabla ya wanandoa hao kukutana, mke wa Feng alikuwa amefanyiwa upasuaji wa urembo (cosmetic surgery) uliogharimu $100,000 nchini Korea Kusini na ndio maana watoto waliozaliwa walikuwa tofauti na wazazi.

Feng
alimshitaki mke wake kwa kuficha ukweli huo na kumfanya amuone mrembo.
Kutokana na maelezo hayo, jaji alimpa ushindi Feng na kumwamuru mke wake
amlipe fidia ya dola $120,000.
Akiongea
na Irish Times, Feng alisema: “Nilimuoa mke wangu kwa upendo, lakini
mara baada ya kupata mtoto wa kwanza tulianza kuwa na migogoro. Binti
yetu alikuwa mbaya haswaa, hadi kufikia wakati akawa ananitisha.”