skip to main |
skip to sidebar
MLEMAVU AIOMBA JAMII KUACHA TABIA YA KUWAFICHA WALEMAVU

JAMII
imetakiwa kutowaficha watu wenye ulemavu bali iwajengee uwezo wa
kufanya kazi kwa kuwatengea maeneo na siyo kuwaacha wakiwa omba omba
mitaani na wengine kufungiwa majumbani.
Rai hiyo imetolewa jana
na Mlemavu wa Viungo, Damas Sanga(48) mkazi wa Igurusi Wilayani Mbarali
Mkoa wa Mbeya wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya
kukutwa akiomba msaada katika baadhi ya Ofisi Mkoani Jijini hapa.
Sanga alisema si kila mlemavu anastahili kubweteka na kusubiri kupewa
misaada na kuomba omba mitaani bali wengine wanauwezo wa kufanya kazi za
ujasiliamali kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kiakili.
Alisema hivi sasa yeye binafsi anauwezo wa kufanya kazi ya ufundi vyuma
hivyo ameamua kuomba msaada ili aweze kununua baadhi ya vifaa
vitakavyomsaidia katika kazi yake hiyo ili aondokane na kuwa tegemezi
kwa kujitafutia riziki yake yeye mwenyewe.
Alivitaja baadhi ya
vifaa vinavyohitajika kuwa ni pamoja na Jenereta kubwa, Inveta na Kabwe
kwa ajili ya shughuli ya kuchomelea vitu vinavyogharimu Shilingi 390,000
ambapo hadi sasa amefanikiwa kupata shilingi 290,000 alizochangiwa na
wasamaria wema hivyo kubakiwa na Shilingi 100,000/= tu.
Mjasiliamali huyo mwenye ulemavu wa miguu alisema hivi sasa anafamilia
ya mke mmoja na watoto wanne ambao hawezi kuwahudumia bila kuwa na kazi
ya kumwingizia kipato na ndiyo maana anaomba msaada ili aweze kuendesha
shughuli zake na kujipatia kipato kitakachoweza kuhudumia familia.
Alisema kwa mtu yeyote atakayeguswa na hali yake awasiliane naye kwa
simu namba 0764 036150 au afike nyumbani kwake Shule ya Msingi Igurusi
Wilayani Mbarali Mkoani hapa kwa msaada wa hali na mali.
Na Saimen Mgalula, Eddy Blog, Mbeya
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi