MKUTANO WA MAJUMUISHO YA ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MAJI ALIYOIFANYA MKOANI DODOMA KUKAGUA MAENDELEO YA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjUI2J-dqpnqdao8_ozNa-CSqKh5ah5gA9pWUe9DN3UhBcOQEA-efHSDOu2nDt4EhuSAyvY_vdw3YNp_D2xHPoRTPYm8pGs12Ypx3K9kZYiDcOp4BD5ftb-EszyndcG91MPgatPKDP-8gu5/s1600/20131116_150519.jpgNaibu Waziri wa Maji Mhandisi Binilith Mahenge (katikati) akitoa maagizo juu ya miradi ya maji kwa wakurugenzi na Wahandisi wa Maji wa wilaya za Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya Naibu Waziri huyo aliyoifanya wiki nzima alipotembelea miradi ya maji mkoa wa Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi na kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Mhe. Jumanne Ngede.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOlz2Wagwy4QZDAGfh-8qmbqNZghsDvS0kMTAvztwZqxPPl9kFYw-0Sub0bhmY1zmgGUx973xc3pzDjVoeMWe3XQ2Q2SfUILyoF_iTleTD9lVopuAY_R745umjG0r9oa1u8cjcdtKvUKfu/s1600/20131116_150558.jpgWadau na viongozi wanaosimamia sekta ya maji Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Naibu waziri wa Maji akitoa majumuisho ya ziara aliyoifanya wiki nzima kukagua utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Dodoma.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh5Q00b8XkerwWQykvtt7x5G2shBrijfBGNwtXi0GASk1FzYu8vJEFPkdASs_7VtZHes0zJnVh6y2s97lEXYMoJ_a1w51_N498Xz4WPHvtaS31THSmn_-ZPd6Iq0vWhKv75GZwPVJ2q7Lbw/s1600/20131116_150629.jpgBaadhi ya wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za Wilayaza Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji (hayupo pichani) wakati wa majumuisho ya ziara aliyoifanya mkoani Dodoma kukagua maendeleo ya utekelezaji miradi ya maji. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mpwapwa Bi. Mwajina Lipinga, Mkurugenzi wa Bahi Bi. Rachel Chuwa na Mkurugenzi wa Kongwa Bi. Bibie Mnyamagoha.
=======
Alasiri ya Jumamosi Novemba 16, alikutana na Viongozi wa Mkoa na Watendaji/wataalamu wanaosimamia Sekta ya maji mkoani Dodoma kwa ajili ya majumuisho ya ziara nzima. Mkutano huo wa Majumuisho ulifanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Dodoma.

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Binilith Mahenge (katikati) akitoa maagizo juu ya miradi ya maji kwa wakurugenzi na Wahandisi wa Maji wa wilaya za Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya Naibu Waziri huyo aliyoifanya wiki zima alipotembelea miradi ya maji mkoa wa dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi na kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Mhe. Jumanne Ngede.

na Issa Michuzi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo