|
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiwasikiliza wawasilishaji
toka Manispaa ya Temeke.
Picha
na Hassan Silayo-MAELEZO
|
Na Frank Mvungi Maelezo
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke yatenga zaidi ya
shilingi milioni 434 katika bajeti ya 2013/2014 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa
vya usafi wa mazingira.
Hayo yamesemwa naAfisa Afya Mkuu wa Manispaa ya Temeke
Bw. Ernest Mamuya leo Jijini Dar es
salaam wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa
Idara ya Habari MAELEZO.
Alisema manispaa hiyo imeweza kuendesha ukaguzi katika maeneo ya kutolea huduma kama hoteli
na katika makazi ya watu ili kuwabaini wanaochafua mazingira.
Katika kufanikaisha suala la usafi katika manispaa
hiyo vifaa vitakavyonunuliwa ni Compactor 1,tela moja la futi 40 kwa ajili ya
usafirishaji taka,ununuzi wa mashine 3 za kusafishia barabara,kununua gari 1 la
maji taka na kujenga vizimba 3 vya kuhifadhia taka kwa muda.
Ambapo katika kuhakikisha halmashauri inaongeza
kiwango cha udhibiti taka na kuboresha hali ya usafi halmashauri imenunua
malori mapya 3 aina ya TATA katika bajeti ya 2012/2013 ambayo yaligharimu
milioni 324.
Bw. Mamuya alibainisha kuwa manispaa hiyo ina mikakati
mbalimbali ikiwemo kusafisha maeneo
muhimu ikiwa ni pamoja na barabara kuu,maeneo ya wazi, masoko, mifereji na kuongeza uwezo wa kukusanya
taka,kuzihifadhi na kuzisafirisha kwenda dampo.
Alisema kuwa Mkakati
mwingine ni kuelimisha na kuhamasisha jamii ili iweze kuunga mkono na kushiriki
katika kuweka mazingira katika hali ya usafi.
Aliongeza kuwa Halmashauri hiyo imefanikiwa kuzuia
magonjwa ya milipuko kwa kipindi cha
miaka mitatu mfululizo kufuatia mikakati kabambe ya kuhamasisha na kusimamia
usafi wa Mazingira katika ngazi ya Kaya na kuigawa halmashauri hiyo katika
kanda 5 za ufuatiliji na usimamizi wa usafi wa mazingira ili kurahisisha kazi
ya ufuatiliaji na usimamizi wa usafi.
Naye Afisa Habari wa Manispaa ya Temeke Lynn Chawala
alisema Manispaa hiyo inatarajia kubadili utaratibu wa kutupa taka dampo la pugu
na kwenda kutupa Kisarawe II
ambapo ni karibu zaidi hali itakayopunguza gharama za kusafirisha taka.