MAMIA WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU DKT. MVUNGI KAREMJEE DSM

Mamia ya  wakazi  wa jiji la Dar es salaam pamoja na viongozi mbalimbali wamejiokeza kutoa heshima za mwisho  kwa aliyekuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba  Dk.Sengondo  mvungi aliyeuawa  na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi huku serikali ikitakiwa kuhakikisha inatafuta ufumbuzi wa kina wa kukomesha matukio kama hayo kwa raia wake.

Licha ya kuwepo na mvua kubwa katika viwanja wa Karimjee  waombelezaji hao walishiriki katika shughuli za kutoa heshima za mwisho sambamba na ibada maalum iliyoongozwa  na Monisinyori Deogratius Mbiku,Paroko wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam  ambaye amesema kila mtu atakufa na hivyo ni bora wajiandae.

Akitoa salamu  za rambirambi  Mwenyekiti wa NCCR -Mageuzi  Mh.James Mbatia amesema matukio kama haya yamekuwa yakitokea kila mara huku serikali ikitoa ahadai ambazo hazitekelezeki hivyo muda umefika ichukue hatua.

Aidha mwenyekiti wa tume ya  marekebisho ya katiba  Mh jaji mstaafu Joseph Warioba amesema tume imepata pigo kubwa huku profesa paramagamba kabudi akisoma wasifu wa marehemu  ambapo amesema  marehemu alikuwa ni sauti ya  kwanza  kudai katiba mpya.

Makamu wa rais Dk Gharib Bilal ni miongoni mwa viongozi wa serikali waliokuwepo katika msiba huo ambapo kwa niaba ya rais ametoa salamu za serikali ambapo amesema  Dk Mvungi ameondoka wakati nchi bado inahitaji mchango wake.

Kwa upande  familia  ya Mvungi wameshukuru kwa namna ambavyo jamii imejitolea katika msiba wa mpedwa wao na kwa hali hiyo wamesema wamefarijika sana na kumwelezea baba yao kama mtu ambaye  hakuwa muoga  na aliweka mbele utaifa  huku baadhia ya waombolezaji wakieleza namna marehemu alivyokuwa na mchango mkubwa  wa jamii  hasa vijana waliokuwa wanasoma masomo ya sheria


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo