INASIKITISHA: WAWILI WAFA BAADA YA KUTUMBUKIA CHOONI KIBAMBA, DAR

WATU wawili wamepoteza maisha baada ya kudondoka kwenye shimo la choo lililokuwa wazi eneo la Kibamba Hospitali, jijini Dar es Salaam! 

Mmoja kati ya marehemu hao alikuwa akijenga ghorofa ndipo alipoteleza na kutumbukia katika shimo hilo lenye maji ambalo litatumika kama choo cha ghorofa hilo. 

Baada ya tukio hilo, rafiki yake alijaribu kumuokoa fundi huyo lakini kwa bahati mbaya naye alitumbukia shimoni humo na wote wawili kupoteza maisha. 

Mmoja wa marehemu hao ametambulika kwa jina moja la Bakari.

Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi. Amen!

-GPL-


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo