Polisi wa mikoa ya Pwani na Kinondoni wanaendesha msako na upelelezi
kubaini ukweli wa taarifa za uwepo wa idadi kubwa ya watoto,
wanaoshikiliwa mateka na kuteswa katika msitu mmoja huko Kibaha mkoa wa
Pwani.
Msako huo unafanyika kufuatia taarifa zilizotolewa na watoto wawili wakazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam ambao walipotea kwa muda mrefu na kupatikana mjini Kibaha, ambapo baada ya kupatikana walidai kuwepo kwa wenzao wanaoshikiliwa mateka na kuteswa msituni.