Watu 16 wanaosadikika kuwa wahamiaji haramu kutoka nchini Ethiopia,
waliokua katika harakati za kusafirishwa kwenda Afrika kusini wametiwa
mbaroni na jeshi la polisi kanda maalum ya Dar-es-Salaam eneo la Makongo
juu manispaa ya Kinondoni
Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai kanda maalumu
ya Dar-es-Salaam kamishina msaidizi wa polisi ACP Ahamedi Msangi amesema
kuwa kutiwa mbaroni kwa watuhumiwa hao, kunafuatia taarifa kutoka kwa
wananchi wenye uzalendo, baada ya kutilia mashaka watu waliokuwa
wamejifungia ndani nyumba iliyokuwa ikiendelea ujenzi.
Awali kamanda Msangi amesema kuwa wanamshikilia
bwana Moshi Majungu anayedaiwa kuwa ni rafiki wa karibu na mchumba wa
bwana Moshi Majungu, Bi Salome anayedaiwa na wahamiaji haramu kuwa ndiye
bosi wao aliyekuwa akiwahudumia kwa chakula, ambapo kamera ya ITV
imeshuhudia matandiko na chupa za mkojo na kinyesi katika jengo hilo.
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida kamera ya ITV
ilishuhudia Kibanda cha kufugia kuku cha jirani na bwana Moshi Majungu,
alichokuwa amejificha mtuhumiwa huyo, baada ya jaribio lake la kutaka
kuwakimbia polisi waliokuwa wameweka mtego ili kumkamata, nao baadhi ya
wananchi na mjumbe wa nyumba kumi katika eneo hilo,bwana saidi
Makilikiti wamesema kuwa bwana Moshi Majungu amekuwa na tuhuma za
kiutapeli katika mtaa wao na kuwa ana kesi katika vituo vya polisi
jijini.
chanzo:ITV