SNURA MUSHI AZUNGUMZIA SAKATA LA PICHA ZA KIMAHABA BAINA YAKE NA MRISHO NGASSA

Snura Mushi afunguka baada ya picha zake za 'kimahaba' na Mrisho ngassa kunaswa mtandaoni
Baaada ya Staa wa sinema na muziki Bongo, Snura Anton Mushi na Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa kunaswa kimahaba hapo jana, leo Mwanadada Snura Mushi amfunguka na kudai kuwa Ngassa ni rafiki yake tuu na si vinginevyo

“Nimeshtuka sana kusikia hizo picha zimewafikia kwa sababu mimi na Ngassa ni marafiki na yeye (Ngassa) ni shabiki mkubwa wa nyimbo zangu.
Ngassa alinitembelea kama marafiki wengine wanaokuja nyumbani kwangu. Simu yangu ilipotea ndiyo maana picha zikavuja lakini ukweli ndiyo huo.”

Kwa upande wake Ngassa ambaye yupo mapumzikoni baada ya kumalizika kwa msimu wa kwanza wa Ligi Kuu Bara hakuweza kusema chochote kufuatia simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa.

Hapo awali ilidaiwa kuwa wawili hao walibambwa wakiwa wamejiachia ‘wakifanya yao’.

Mnyetishaji huyo alidai kuwa wawili hao walikuwa wakiminyana bila kujali macho ya watu waliokuwa wakifika nyumbani kwa Snura hasa marafiki na majirani zake.“Yaani walikuwa wakioneshana mahaba kama njiwa bila kificho chochote.

“Kuna ‘taimu’ Snura alikuwa akimpakata Ngassa utadhani mtoto mdogo.  “Baadaye hata Ngassa naye alifanya hivyohivyo huku akicheza na nywele za Snura anavyotaka,” alidai shuhuda wetu.

Ili kujiridhisha, Tulisaka picha za wawili hao ambazo walikuwa ‘wakijifotoa’ kwa simu zikiwaonesha wakiwa katika mahaba jambo lililozua utata na maswali kwa walioziona.

Uchunguzi ulibainisha kuwa siyo mara ya kwanza kwa Snura na Ngassa kunaswa wakiwa beneti kwani wiki mbili zilizopita walibambwa kwenye ukumbi mmoja wa starehe jijini Dar wakila bata ndefu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo