Na Saimeni Mgalula,EDDY BLOG, Mbeya
Mgogoro kati ya Familia ya maremu Kayuni na chama cha mapinduzi (CCM) katika mji wa Tunduma Wilayani Momba Mkoani hapa,kuhusu mkataba wa Vyumba ulichukuwa sura mpya baada ya chama hicho kubomoa chumba kimoja licha ya kesi hiyo kuwepo mahakamani.
Hayo yalisemwa na Mtoto wa marehemu Agness Kayuni wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la tukio Mwishoni mwa juma ambapo alisema kuwa kitendo kinachofanywa na ccm wilayani hapa sio cha kiungwana kwani wanataka kumdhulumu mama mjane na wanashindwa kukaa meza moja na familia hiyo ili kumaliza mgogoro huo kwa njia ya amani.

Alisema "licha ya kesi hiyo kuwepo mahakamani lakini chama hicho kinawatuma vijana kuvunja vyumba hivyo wakati bado hawajafikia muafaka" alisema mtoto wa marehemu Kayuni.
Mmoja wa mkazi wa Tunduma Joseph Mwachemba alisema kuwa kitendo hicho ni cha kinyanyasaji kwani ccm walitakiwa wakae meza moja ili wafikie muafaka wa jambo hilo.
Mwachemba aliendelea kwa kusema kufuatia vurugu hizo zilisababisha baadhi ya Wafanyabiashara wa Nchi jirani kuogopa kuja hapa Nchini kufanya biashara katika Mji wa Tunduma wakihofia kuwa hakuna Amani.
Mwenyekiti Juma Rashidi (ccm) wa wilayani hapa alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa ni utekelezaji wa amri ya mahakama iliyoamuru kuondolewa kwa wafanya biashara katika jengo hilo baada ya hatua iliyo bakia ni kuhusu chama kuchukua hatua gani dhidi ya jengo hilo.