Mtuhumiwa
wa mauaji Tabu Jumanne (50) mkazi wa Kibaoni Singida mjini (katikati
anayekwepa kamera) akiwa kwenye chumba cha mahakama ya wilaya ya Singida
akisubiri kusomewa shitaka la kuumuawa Fatuma Shaban. Tabu anakabiliwa
na shitaka la kumuuawa Fatuma, akishirikiana na binti zake Halima Swedi
(anayejificha mwenye fulana nyekundu) na Mwamvua Yusuph baada ya
mwanamke huyo kumdai Tabu amlipe mshahara binti yake aliyekuwa akifanya
kazi za ndani.
Askari polisi wakiwa na mahabusu wakiwapeleka mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Singida kusomewa mashitaka yanayowakabili.(Picha na Nathaniel Limu).
======
Na Nathaniel Limu, Singida
Mwanamke
mmoja mwenye umri wa miaka 50 na watoto wake wawili wa kike wakazi wa
Kibaoni mjini Singida wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya
ya Singida wakituhumiwa kumuuawa Fatuma Shaban maarufu kwa jina la mama
Rabeca.
Washitakiwa hao ni Tabu Jumanne na binti zake Halima Swedi na Mwamvua Yusuph.
Mapema
Mwendesha Mashitaka Sajenti wa Polisi Godwel Lawrance alidai mbele ya
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Singida, Flora Ndale kuwa mnamo
julai nne mwaka huu majira ya jioni huko katika kitongoji cha Mahembe
kata ya Kinadi Manispaa ya Singida washitakiwa kwa pamoja walimpiga
Fatuma Shaban sehemu mbalimbali za mwili wake.
Lawrance amesema kipigo hicho kilisababisha kifo cha Fatuma pale pale.
Washitakiwa
hawakutakiwa kujibi cho chote kwa vile Mahakama hiyo ya Wilaya haina
mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena
Novemba sita mwaka huu.
Kwa
mujibu wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa siku ya tukio Fatuma alienda
nyumbani kwa mshitakiwa Tabu kudai fedha za mshahara wa binti yake
aliyekuwa ameajiriwa kufanya kazi za ndani.
Inadaiwa
kitendo cha Fatuma (marehemu) kumdai mshitakiwa Tabu malipo ya mshahara
wa binti yake kilizua ugomvi na ndipo Tabu kwa ushirikiano wa binti
zake waliamua kumpiga mama huyo na kusababisha kifo chake papo hapo.