Katibu wa Njombe Press Club(NPC) Hamis Kassapa(kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao cha wanachama wa chama hicho cha kupitisha katiba, kulia kwake ni mwenyekiti wa NPC Mercy James.
Wanachama wakifuatilia kikao
======
Wajumbe wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe, Njombe Press Club (NPC) hii leo wameipitisha katiba ya chama hicho katika mkutano mkuu uliofanyika katika ukumbi wa Dosmeza mkoani Njombe
Hatua hiyo imetokana na wajumbe hao wakiongozwa na mwenyekiti wa NPC Mercy James na katibu Hamis Kassapa, kupitia hatua kwa hatua kila kipengele kilichopo kwenye katiba hiyo ili chama hicho kizidi kufanya kazi kwa uimara zaidi
Kupitishwa kwa katiba hiyo kumezidi kukiimarisha chama hicho kizidi kufanya kazi zake chini ya misingi ya kisheria ya chama na nchi kwa ujumla
Katika hatua nyingine chama hicho kwa pamoja kimedhamiria kuwa mialiko ya shughuli mbalimbali hasa za kiserikali zikiwemo ziara za viongozi mbalimbali, kupitia kwenye chama na si vinginevyo kutokana na kuwepo kwa mikanganyiko ya waandishi wa habari ambao ni wanachama kwenda kienyeji kwenye shughuli mbalimbali bila idhini ya chama
Aidha wamesema wataandika barua kwa taasisi mbalimbali kuzitaarifu kuhusu suala hilo ili lianze mara moja