Waandaaji
wa shindano la kusaka vipaji vya uimbaji la tusker project fame
wameelezea kufurahishwa na mwitikio wa wasanii mbalimbali waliojitokeza
katika usaili kwa ajili ya kuwania nafasi ya kuiwakilisha tanzania
kwenye mashindano hayo.
Zaidi ya wasanii 150 wamejitokeza katika usaili uliofanyika jijini
dar es salaam ambapo kutokana na vipaji vya hali ya juu vilivyooneshwa
na wasanii hao majaji wamekuwa na kazi ngumu ya kuchagua wasanii watatu
tu kati yao ambao watapeperusha bendera ya tanzania katika mashindano ya
tusker project fame huku pia yakishirikisha washiriki kutoka kenya,
uganda, sudan kusini na burundi.
Nao baadhi ya wasanii waliopata fursa ya kuzungumza na itv wamesema
mashindano hayo yatawasaidia kuinua vipaji vyao ikiwa watapata fursa ya
kuingia kwenye jumba la tusker project fame hivyo wamewaomba sapoti ya
watanzania katika kila hatua watakayofikia kupitia mashindano hayo.