Mkuu
wa majeshi jenerali Davis Mwamunyange amesema vikosi vya jeshi la
wananchi nchini vinapaswa kuendeleza utaratibu wa mazoezi na mafunzo ya
mara kwa mara ili kujiweka imara kwa ulinzi wa ndani na nje ya nchi.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mazoezi ya vikosi vya nchi kavu katika brigedi
ya mbuni yaliyopewa jina la operesheni ''kuwa imara
''jenerali mwamunyange amesema jeshi la tanzania limejenga heshima ya kimataifa hivyo ni lazima kuitunza heshima hiyo.
Naye
meja Jenerali Salum Kijuu ambaye ndiye mkuu wa vikosi vya nchi kavu
anasema lengo la mazoezi hayo ni kuwandaa maafisa na askari kimafunzo
ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na adui katika mapigano ya nchi
kavu.
Kuhusu uhusiano wa kijeshi baina ya nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo nchi ya Rwanda,mkuu wa operesheni na Mafunzo
kamandi ya jeshi la nchi kavu brigedia jenerali Zoma Kongo anasema
uhusiano ni mzuri na nchi hizo zimeendelea kushirikiana katika
mafunzo mbalimbali ya kijeshi