KAMBI YA UPINZANI BUNGENI YATISHIA KUTOUNGA MKONO MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA KATIBA 2013



Kambi ya upinzani bungeni imesema kutokana na mtafuruku uliotokea bungeni kwa kutolewa nje kiongozi wa kambi hiyo Mh. Freeman Mbowe amesema hawaungi mkono muswada  wa sheria ya marekebisho ya katiba ya mwaka 2013 kwa kuwa  haiwatendei haki watanzania.

Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari katika ukumbi wa Pius Msekwa bungeni mjini Dodoma kuhusiana na mtafuruku uliotokea bungeni kiongozi huyo wa kambi ya upinzai bungeni Mh Freeman Mbowe amesema hawatashiriki katika mjadala huo kwa kile walichodai kuwa chama cha mapinduzi (CCM) kina ajenda ya siri na kushiriki kwao hawatakuwa wanawatendea haki watanzania 

Akizungumzia juu ya kile kinachoonekana kwa sasa kuwa ni uhusiano mwema baina ya chama cha wananchi (CUF) na Chadema,mbunge wa Mkanyageni kupitia CUF  Mh Habib Mnyaa amesema siasa haina adui wala rafiki wa kudumu na hivo wameungana na Chadema katika kutetea haki,usawa na maslahi ya wananchi wa Zanzibara na wale wa Tanzania Bara

Katika tukio jingine  wanasheria wa masuala ya haki za binadamu wamesema kilichotokea bungeni ni kutokana na kitendo cha naibu spika kuchelewa kutoa majibu ya miongozo kama ilivyoombwa na baadhi ya wabunge na kuwafanya wabunge wa upinzani kuona wanaburuzwa na kuamua kutoka nje na kuongeza kuwa hawakufurahishwa na jambo hilo kwa kile alichodai kuwa mawazo yawachache yanapigwa kumbo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo