SEMINA YA KAMATA FURSA YAWAFURAHISHA WAKAZI WA IRINGA

Wakazi  wa mji  wa Iringa  wakiwa katika semina ya  kamata  Fursa leo
Mwakilishi  wa Max malipo  akitoa  maelezo ya jinsi  walivyokuza ajira  nchini
Mmoja kati ya  wawezeshaji  katika  semina ya kamata  Fursa  inayoendeshwa na kituo  cha  radio  Clouds Fm ,msanii Nickson simon a.k.a Nikki wa  pili  wa  pili akieleza  fursa  zilizopo na changamoto  zake.
 ...................................................
MSANII  Nickson simon a.k.a Nikki wa  pili   amewataka  vijana  nchini  kuepuka   kukimbilia  mijini na badala  yake  kutumia  fursa  zilizopo katika maeneo yao  kama  njia ya  kujikwamua  kiuchumi.

Kwani  alisema  kuwa lengo  La  semina  hiyo ya  kamata  Fursa  imelenga  kubadili  mitizamo   ya  jamii  hasa  vijana  katika  kuwawezesha  kubadili  mitizamo  yao   ili  kuweza kujipatia  maendeleo .
Msanii  Nikki   wa  pili ameyasema hayo  leo  katika  ukumbi  wa  st.Dominic  katika  warsha  ya  siku  moja ya  kamata  fursa  iliyoandaliwa na  kituo  bora  cha  radio  Clouds Fm
Alisema   kuwa mbali ya  viongozi  wa kada  mbali mbali  kuzungumzia  suala la  fursa  ila  bado watanzania  waliowengi bado  hawajabahatika  kuiona  fursa  hiyo.
Hivyo  alisema  kuwa  warsha   hiyo  imelenga pia  kuwawezesha  watanzania  kuanza  kuziona  fursa  zilizopo  na ikibidi kuweza  kuzitumia  fursa  hizo.

“ Tunapinga  mawazo ya  vijana  ambao  wanatoka vijijini na  kukimbilia  mijini kwenda  kutafuta  fursa  mbali  mbali   huku  wakiwa  wameacha  fursa  zilizopo katika  maeneo  yao ambayo  wanaishi”
Hata  hivyo  amesema baada  kuzunguka katika maeneo  mbali mbali ya nchini ikiwemo Kigoma , Tabora ,Mtwara  , Mbeya  na  Iringa   wamebaini  kuwa  tatizo  kubwa  ni  thamani  ndogo  ya mazao yanazozalishwa  katika maeneo  hayo.

Mbali ya  kutaka thamani ya  mazao  hayo  kuongezwa  bado  alisema  sehemu  kubwa  ya  wazalishaji  mali ni  wazee  huku  vijana  wengi  wamekuwa  wakikimbilia  mijini  na kuwa  iwapo wataongeza thamani  ya mazao  kuna  uwezekano  wa vijana  wengi  kuepuka  kukimbilia mjini
“ Vijana  lazima kufanya  tafiti  ili kuona  ni namna  gani unaweza  kupata  bei  ya  bidhaa mbali mbali  na baada ya  hapo  kujiunga katika  vikundi  vya  kiuchumi ili  kuweza  kupata  mikopo “
Pia  alisema  zipo  taasisi nyingi  ambazo zinatoa  mikopo katika makundi  mbali mbali  na moja kati ya taasisi  hizo ni pamoja na  NSSF ambao  wanatoa  mikopo  ya  zaidi ya Tsh bilioni  1 katika  vikundi.
 
chanzo: mzee wa matukio daima


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo