MWANAMUME mmoja kaunti ya Murang’a alinusurika kifo baada ya mkewe kumlazimisha kunywa sumu.
Bw Charles Mbaruku Kimani kutoka
kijiji cha Matongu katika lokesheni ya Kimathi eneo la Kiharu KENYA alidai
mkewe alimpiga dafrau usiku na kutaka kumnywesha sumu kwa nguvu lakini
akakataa.
Akiongea na Taifa Leo Ijumaa
katika kituo cha polisi mjini Murang’a ambapo aliandikisha ripoti,
jamaa huyo wa miaka 54 alidai mkewe ana mazoea ya kumshambulia
akishirikiana na mwanawe wa kiume.
Bw Kimani alisema wameoana kwa miaka
13 na wamekuwa wakizozana kwa siku nyingi huku mkewe akitoroka kwa
wazazi wake mara kadhaa katika kijiji cha Kimicha kaunti jirani ya
Kirinyaga.
Alisema kuwa siku ya Jumamosi usiku,
mkewe alichanganya dawa ya kuua kupe na kuitia kwenye chupa na kumkaba
koo mzee huyo huku akitaka anywe dawa hiyo ili afe.
“Tulikuwa tumetoka safari na ndani
ya nyumba kulikuwa na giza kwani hatukuwa tumewasha taa na nilikuwa
nimeketi kitini wakati mke wangu aliponishambulia,” alisema Bw Kimani
ambaye alitibiwa hospitali kuu ya Murang’a baada ya kisa hicho.
Mwanamme huyo ambaye anafanya
biashara ya kuuza changarawe alidai mkewe alimshika kwenye sehemu ya
shingo na kuelekeza chupa hiyo iliyojaa sumu kwenye mdomo wake lakini
mwanamme huyo akamuuma mkewe mkono wakati wa kisa hicho