Leo ni mwaka mmoja tangu aliyekuwa mwandishi wa habari wa channel 10 marehemu Daudi Mwangosi kuuawa na kitu kinachosadikika kuwa ni bomu katika eneo la Nyololo wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa tarehe 2.9.2012
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa mtandao huu wa EDDY BLOG na katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Francis Godwin, wamejipanga kufanya maandamano ya amani katika manispaa ya Iringa kukumbuka kifo cha mwandishi huyo mkongwe kuanzia saa tatu asubuhi
Katika maandamano hayo ya amani wamewaalika waandishi wa habari pamoja na wadau wa sekata ya habari kujumuika pamoja kukumbuka kifo hicho cha Daudi Mwangosi
Mungu azidi kumpa pumziko la milele marehemu Daudi Mwangozi, ameen
