Najua wengi mmemmisi msanii huyu na mnazikumbuka kazi zake ikiwemo (Umaskini huu) kazi ilomzolea kitita cha mashabiki Ndani na nje ya nchi..
Kwa sasa msanii huyu amekaa kimya kwa mda mrefu kidogo baada ya kuachia kazi iliotambulika kwa jina la (Sumu ya panya)
aliamua kujichimbia na kuendelea kufanya maandalizi ya kulipa deni kwa
mashabiki wake yani kuwapa burudani na ujumbe kama ilivyo ada,
Akiongea
na mwandishi wetu hakutaka kufunguka
sana kuhusu ujio wake wa sasa bali alizungumza kwa ufupi tu kwamba kuna
vitu anaviandaa yeye na mwenzie ''Joni woka'' yani kwa ujumla kundi lao
la (WA2KU2) Linaloundwa na wasanii wawili ''Ras Lion'' na ''Joni woka'' sasa lipo katika maandalizi ya kazi kali hivyo mashabiki wasijali wasubiri burudani.
