Zaidi
ya magari ya mizigo 400 yaliyokuwa yamekwama katika eneo la Rusumo
mpaka wa Tanzania na nchi ya Rwanda baada ya serikali ya Rwanda
kupandisha kodi ya kutoka dola 152 hadi dola 500 kwa kila gari moja la
mizigo na kusababisha msongamano mkubwa mpakani
Hapo
yameanza kupita kufuatia tozo hiyo mpya kusitishwa ambapo magari mengi
yanapita Rwanda kwenda Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Wakizungumza kabla ya kuruhusiwa baadhi ya madereva wa magari ya mizigo
wameiomba serikali ya Rwanda kufanya makubaliano na nchi wanachama wa
afrika mashariki kwa kuwa na lugha moja ya kodi na kwamba marumbano
yaliyopo kati ya rais wa nchi ya Rwanda na Tanzania na kwamba rais wa
Rwanda amepandisha gharama bila taarifa kwa wasafirishaji hali
inayosababisha usumbufu kwa madereva.
Kwa
upandewake mmoja wa watendaji wa serikali wa Mamlaka ya mapato
Tanzania(TRA) aliopo katika eneo la mpaka wa tanzania na nchi ya Rwanda
Bw. Nasoro Ibrahimu amekili kuwepo kwa msongamano mkubwa wa magari ya
mizigo katika eneo la tanzania baada ya kuzuiliwa kuingia katika nchi ya
Rwanda hali iliyosababisha kufunga barabara ya rusumo ngara isipitike
CHANZO: ITV