Washiriki
wa tamasha la 11 la mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP)
wakishiriki maandamano ya amani ya maadhimisho ya miaka 20 ya
mapambano ya ukombozi wa wanawake kimapinduzi. (Picha zote na Francis
Godwin wa matukio daima)
Waadamanaji hao wakiwa na mabango yenye jumbe mbali mbali
Tamasha
la 11 la mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) limeanza kwa
maandamano katika ofisi za TGNP eneo la Mabibo jijini Dar es
Salaam.
Maandamano hayo yameanzia lango kuu la ofisi za TGNP na kuhitimishwa katika viwanja vya tamasha eneo hilo la TGNP.
Akizungumza katika uzinduzi wa tamasha hilo mkurugenzi wa TGNP
Usu Mallya alisema wakati TGNP inaazimisha tamasha hilo bado
inajivunia mapambano makubwa yaliyodumu kwa miaka 16 katika
kupigania jengo hilo ambalo lilikuwa na kesi mahakamani hadi
wanaposhinda kesi hiyo.
Hivyo alisema ushindi wa kesi hiyo dhidi ya jengo hilo
utawafanya sasa kuendelea kuboresha zaidi jengop hilo na
kulifanya kuwa la kisasa zaidi na kuendeleza mafunzo mbali mbali