HOTUBA YA MHESHIMIWA
MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI WA
KUTOA HOJA YA KUAHIRISHA MKUTANO WA KUMI NA MBILI WA BUNGE, DODOMA TAREHE 06
SEPTEMBA, 2013
I. UTANGULIZI:
a)
Maswali
1.
Mheshimiwa Spika, nianze kwa
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kutekeleza na kukamilisha majukumu
yetu katika muda uliopangwa. Katika Mkutano huu Maswali 120 ya Msingi na 305 ya
Nyongeza ya Waheshimiwa Wabunge yalijibiwa na Serikali. Aidha, jumla ya Maswali
12 ya Msingi ya Papo kwa Papo na 11 ya Nyongeza yalijibiwa na Waziri
Mkuu.
b)
Miswada
2.
Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huu,
Bunge lako Tukufu lilijadili na kupitisha Miswada Mitatu (3). Miswada hiyo ni:
i)
Muswada wa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji wa
Mwaka 2013 [The National Irrigation Bill, 2013];
ii)
Muswada wa Sheria wa Vyama vya Ushirika wa
Mwaka 2013 [The Cooperative Societies Bill, 2013]; na
iii)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2013 [The Constitutional Review (Amendment) Bill,
2013].
3.
Mheshimiwa Spika, napenda nitumie
nafasi hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa kujadili na kukubali kupitisha
Miswada hiyo kwa umahiri mkubwa. Aidha, niwapongeze Mawaziri na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali pamoja na Wataalam wote waliohusika na Maandalizi ya Miswada
hiyo. Kipekee niwashukuru Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa kupitia
Miswada yote na kutoa maoni yao, ambayo sehemu kubwa yamezingatiwa na Serikali
katika kuboresha Miswada hiyo.
4.
Mheshimiwa Spika, asubuhi ya leo Bunge
lako Tukufu lilipokea Kauli za Mawaziri wa Fedha na Uchukuzi. Wote
tunawashukuru kwa maelezo yao.
II.
UTEKELEZAJI
WA MFUMO WA MATOKEO MAKUBWA SASA “BIG
RESULTS NOW”
ENDELEA KWA KUBOFYA HAPA>>>>>>>>>>>>
