ZAIDI YA FILAMU 20 KUONESHWA DAR FILAMU FESTIVAL

Dar FilamuFestival-logo 532
Tamasha kubwa la Dar Filamu Festival.

TAMASHA kubwa na la kipekee la Dar Filamu Festival (DFF) linatarajia kuonyesha filamu zaidi ya 20 katika viwanja vya CoICT- UDSM- Posta Kijitonyama kuanzia tarehe 24 September 2013 , filamu zitachaguliwa kutoka filamu zaidi ya mia mbili ziliomba kuonyeshwa na wamiliki wa filamu hizo kazi zitakazoonyeshwa zitakuwa zile zilizopendekezwa na bodi ya DFF.

Filamu ya Black Tshirt
Black Tshirt moja kati ya filamu za Swahilihood’
Omega Confusion
Filamu ya Omega Confusion
Dar Filamu Festival
Dar Filamu Festival 2013

Akiongea na FC mkurugenzi wa Haak Neel Production Godfrey katula amesema filamu zitakazoonyeshwa ni zile ambazo zimeonekana kupendwa na kukidhi vitu mbalimbali kama maadili utamaduni, ubora wa filamu (Quality), sauti nzuri filamu zilipitia katika taasisi husika pia kutakuwa na kazi zilizofanya vizuri sokoni.

“Dar Filamu Festival ni tamasha linalowakutanisha wadau wa filamu nchini kwa kujadili masuala ya tasnia ya filamu, lakini pia ni wakati wa kujitangaza kupitia kazi hizo, jambo lingine ni kuleta mwamko wa wapenzi wa filamu kujenga utamaduni wa kuangalia filamu katika majumba ya sinema yaliyokuwepo,”anasema Goddy.

Tamasha la Filamu la Dar Filamu Festival (DFF), litaanza rasmi tarehe 24/September/2013 hadi tarehe 26 kwa kila siku filamu zitaanza kuruka saa 12 jioni hadi saa sita usiku ulinzi wa kutosha kutoka kwa makampuni ya kimataifa wakishirikiana na Polisi huku filamu hizo zikirushwa kupitia Projector kubwa One air mtazamaji akipata filamu safi bila kufinya macho kwani utaiona live.

CHANZO:FC


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo