skip to main |
skip to sidebar
DALADALA KWA AJILI YA WANAWAKE TU ZATUA DAR
Kampuni ya Simon Group, imekabidhi mabasi 40 kwa Shirika la
Usafirishaji Dar es Salaam, (Uda) ili kurahisisha usafiri Jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari katika sherehe ya
uzinduzi wa mabasi hayo jijini Dar es Salaam, jana Mwenyekiti Mtendaji
wa Simon Group, Robert Kisena, alisema huo ni mpango wa muda mfupi wa
uwekezaji na uendelezaji katika shirika la Uda, lengo ikiwa ni kuingiza mabasi mapya mengine 2000 ifikapo Juni, 2014.
Kisena alisema vile vile Uda limeingia ubia na Kampuni za Africarriers
na Eicher wa kununua mabasi hayo 2,000 ifikapo Juni mwakani.
Kisena aliongeza kuwa huo ni mpango wa muda mfupi wa uwekezaji na
uendelezaji wa Uda wenye nia ya kuboresha huduma ya usafiri kwa wakazi
wa Jiji la Dar es Salaam, ambapo katika mpango wa muda mrefu ni kuingiza
magari mengine 5,000 na kufikisha idadi ya magari 7,000 ifikapo mwaka
2017.
“Katika mabasi hayo, pia kutakuwa na mabasi maalum ya
kubeba wanawake pekee, lengo la kuwa na mabasi haya, ni kuwapunguzia
usumbufu akina mama wa Dar es Salaam, ambao kwa muda mrefu sasa wamekuwa
wakiteseka kupigana vikumbo na wanaume katika kugombania usafiri wa
maeneo mbalimbali hapa jijini,” alisema Kisena.
CHANZO:HABARI KWANZA
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi