Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mullugo akiwahutubia wazazi na wanafunzi katika mahafali ya kwanza
kwenye chuo cha KPC Wilayani kyela.
waziri wa uchukuzi Dk Harrison
Mwakyembe ambaye pia ni mbunge wa Kyela akiwa na viongozi kadhaa waliohudhuria sherehe hizo za
mahafali.
IMEELEZWA
kuwa mwamko mdogo wa kielimu kwa Wazazi wa Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya
ndicho chanzo cha kupelekea wilaya hiyo kushika nafasi ya kwanza
kufanya vibaya kimkoa katika nyanja ya elimu nchini.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Phillipo Mulugo wakati wa
mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ufundi na Biashara Kyela (Kyela
Polytechnic College) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki chuoni hapo.
Mh.
Mulugo alisema kuwa wilaya ya Kyela ni miongoni mwa wilaya 40 ambazo
zimekuwa zinafanya vibaya katika suala la elimu na kwamba ni wilaya
ambayo inashika nafasi ya kwanza kimkoa.
Alisema
kuwa kutokana na mwamko mdogo wa wazazi kielimu ndiyo maana chuo hicho
kimekuwa na wanafunzi wachache tofauti na mikoa mingine ambayo imekuwa
na vyuo vichache lakini wanafunzi ni wengi kutokana na wazizi kuhimiza
watoto wao kujikita katika masomo.
“Ni
heri niache ubunge wangu kuliko kuangalia suala baya kama hili
wilayani Kyela likiachwa kama ilivyo kwa kuwa hii ni aibu kwetu sote
hasa wakazi wa Wilaya hii na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla” alisema Mulugo.
Aliongeza
kuwa kutokana na tatizo hilo Serikali imeiingiza Wilaya hiyo kuwa
miongoni mwa wilaya ambazo zimepewa kipaumbele katika utekelezaji wa ‘Big result now’ yaani mambo makubwa sasa ili kuongeza ufanisi katika uchapaji kazi.
Waziri
huyo alisema kutokana na uanzishwaji wa kauli mbiu hiyo na Rais
nilazima viongozi wawajibike ipasavyo katika kusimamia suala hilo na
kudai kuwa ikiwezekana walimu wakuu na maAfisa elimu wawajibishwe iwapo
watathibitika kufanya uzembe katika jambo hili.
Aliongeza
kuwa kunabaadhi ya waalimu Wilayani hapa wamekuwa na kawaida ya kunywa
pombe hasubuhi nyakati za masomo na kufanya vibaya katika vipindi vyao
pindi wanapo fundisha na kuwa amemuagiza mkuu wa Wilaya Magreti Malenga
kuwashughurikia waalimu watakaobainika kufanya hivyo.
“Natoa
agizo kwa Mkuu wa Wilaya kuhakikisha anafuatilia ufundishaji wa walimu
mashuleni kwani kuna baadhi ya walimu wamekuwa wakinywa pombe majira ya
asubuhi tena wakati wa kazi jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya
elimu kwa watoto” aliongeza Mulugo.
Kwa
Upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dkt Salatiel Mwakyambiki alisema kuwa
Kyela inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya Biashara ndogo ndogo
na matumizi ya simu wawapo darasani ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa
kurudisha nyuma maendeleo ya watoto wa kike, na baadhi ya vijana wa
kiume.
Aidha
alitaja changamoto nyingine kuwa ni matumizi ya simu ambapo alisema
kuwa baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakitumia mawasiliano wakiwa darasani
jambo ambalo alisema kuwa limeongeza kupunguza nidhamu kwa wanafunzi.
Mbunge
wa Jimbo hilo Dr,Harrison Mwakyembe kwa upande wake amewataka wazazi
kuwahimiza watoto wao kujikita katika elimu katika kujiunga na vyuo ili
kuondokana na haibu hii ya kuwa wa mwisho kimkoa katika sekta ya elimu
NA IBRAHIM YASSIN