
BAADHI
ya wananchi Wilayani Kyela Mkoani Mbeya wamezipongeza juhudi
zinzofanywa na kanisa la maombezi la Temple of prayer all nations
churh(TPFNC) kwa kazi kubwa inayoifanywa na wachungaji ya kuombea wagonjwa ambao wanapona baada ya kupokea uponyaji kutokana na maombezi yanayofanywa kanisani hapo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti mara baada ya maombezi hayo walitoa ushuhuda ambapo
walidai kuwa wamepata tumaini jipya baada ya watu wanaougua magonjwa ya
hajabu na wale wenyeshida mbalimbali kuondokana na shida hizo pindi
wapatapo maombezi yanayoambatana na upakwaji wa mafuta ya uzima pindi waendapo kanisani hapo.
Dorris
Crement mkazi wa kijiji cha Lupaso kata ya Kajunjumele alisema kuwa
yeye alipata matatizo ya kuvumba mguu tangu mwanzoni mwa mwezi huu na
alizunguka katika hospitali kadhaa na kwa waganga wa tiba mbadala kwa
lengo la kupata tiba lakini hakufanikiwa kupona na kuwa alifika kanisani
hapo baada ya kupewa taarifa na sasa amepona baada ya kufanyiwa maombi
na kupakwa mafuta.
Vessy
potes (13) kutoka kata ya Bujonde ambaye ni mwana funzi wa darasa la
saba shule ya msingi Isanga alisema alianza kusumbuliwa na sikio tangu
mwezi wa sita mwaka huu baada ya kutibiwa katika hospitali ya Wilaya
homa ilizidi na ilipofika siku ya saba ya matibabu yake alipata tatizo
lingine la kupooza na baada ya matibabu ya hospitalini kushindikana
alipelekwa na wazazi wake katika kanisa hilo la maombezi na amepona mara
baada ya kuombewa na kupakwa mafuta ya upako.
Dukra Ngatunga (13) mkazi wa Ilomba Mbeya na ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza Lyoto sekondari
alisema kuwa yeye alifiwa na pacha wake mara baada ya kufa pacha huyo
alimwita ili naye afe wakaishi wote katika sayari nyingine naye
alijikuta akinywa sumu ya panya lakini hakuweza kufa baadaye alitafuta
mabetri matatu ya redio na kuyasaga na kunywa baadaye alilegea lakini
hakufa.
Mama
mzazi wa mtoto huyo Nuru Mwakyeru alisema walipomuona mtoto huyo
walimhoji ambaye naye aliwaeleza kuwa anaitwa na pacha wake
aliyetangulia mbele za haki ili wakaishi wote katika sayari mpya ndipo
walipomkimbiza hospitalini na madaktari walifanikiwa kumchoma sindano ya
kuondoa sumu mwilini lakini waliporudi nyuimbani hali ilizidi kuwa
mbaya.
Aliongeza
kuwa baada ya hali hiyo kuzidi kuwa mbaya waliamua kusafiri hadi
Wilayani Kyela kwa lengo la kupata huduma ya maombezi inayofanywa
kanisani hapo na kuwa walipofika walipokelewa na watumishi wa kanisa
hilo ambao walifanya maombi kwa dadika 15 na kumpaka mafuta ya upako
ndipo hali ya mtoto wake ikaendelea kuimalika na siku iliyofuata akapona
kabisa na kurejea nyumbani.
Mchungaji
wa Kanisa hilo ambaye alijitenga na askofu wake Mullilege mkombo(mzee
wa yesu)na kuanzisha kanisa lake Nabii Charles Mkuvasa alisema kuwa
kanisa lake limekuwa kama hospitali ya rufaa kwa kuwa wagonjwa wengi na
watu wenyeshida mbalimbali wanaokuja kwake wanapona pindi anapowaombea na wao kupokea uponjaji kutoka kwa yesu Kristo.
Mkuvasa
aliongeza kuwa hivi sasa anakosa usingizi baada ya wagonjwa kutoka
mikoa mbalimbali ya Tanzania na wa Nchi jirani ya Malawi wanaofika
kanisani hapo kwa wingi ambao amekuwa akiawafanyia maombi mfululizo
usiku na mchana hivyo kukosa muda wa kupumzika na kwamba hivi sasa
anatarajia kufungua matawi vijijini ili kurahisisha na kusogeza huduma
kwa jamii na jamii hiyo inatakiwa kumshirikisha mungu kwa kila jambo ili
kukwepa majaribu ya Ibilisi.
NA IBRAHIM YASSIN