Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na TLC leo wamemshtaki Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mwanasheria mkuu wa serikali kwa kukiuka Katiba katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Kesi iliofunguliwa katika Mahakama Kuu ni ya kikatiba. Kesi hiyo inasubiri kupangiwa majaji.
Kesi hiyo imefunguliwa katika mahakama hiyo ikiwa ni hatua za kisheria kupinga kauli alioitoa Pinda bungeni hivi karibuni kwamba watakaokiukwa amri za vyombo vya dola ‘wapigwe tu’.
Hivi karibuni Waziri Mkuu, Pinda akiwa bungeni alisema serikali imechoshwa na vurugu zinazotokea mara kwa mara na kwamba hakuna namna nyingine ya kuwadhibiti raia wanaowadhuru vyombo vya dola na kutotii amri zaidi ya kuwapiga.
Awali LHRC ilisema Pinda anapaswa kushtakiwa kwa kuwa amevunja kifungu cha katiba ya Usawa mbele ya sheria ibara 13 (1).