Mashine
maalum ya kufulia nguo aina ya HITACHI iliyotolewa na Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda kwa kituo cha
kulelea mayatima cha Katandala Mkoani Rukwa na kukabidhiwa kituoni hapo
na Katibu wake wa Jimbo Ndugu Charles Kanyanda leo tarehe 30, Agosti
2013. Msaada huo wenye thamani ya Tshs. Milioni moja na nusu (1.5) ni
ahadi ya Waziri Mkuu aliyoitoa alipotembelea kituoni hapo mapema mwaka
huu.
Ndudu
Charles Kanyanda Katibu wa Jimbo wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Katavi
akimkabidhi Mama Mkuu Mariastella Wampembe wa Masista Maria Mtakatifu
Malkia wa Afika ambao ni wamiliki wa kituo cha kulelea mayatima cha
Katandala mashine maalum ya kufulia nguo iliyotolewa na Waziri Mkuu kwa
kituo hicho leo tarehe 30, Agosti 2013.
Mama
Mkuu Mariastella Wampembe wa Masista Maria Mtakatifu Malkia wa Afika
wamiliki wa kituo cha kulea mayatima cha Katandala Mkoani Rukwa akitoa
shukrani zake za dhati kwa Waziri Mkuu kupitia kwa Katibu wake wa Jimbo
Ndugu Charles Kanyanda kwa msaada huo wa mashine ya kufulia. (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)