WAWILI WAKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA MKOANI KATAVI

 
Watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoa wa Katavi  kwa tuhuma za kukamatwa na madawa ya kulevya aina Bangi gunia tatu na mbegu zake kilo mbili  zikiwa zimehifadhiwa nyumbani kwa watuhumiwa 
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  aliwataja waliokamatwa na kushikiliwa na jeshi hilo kuwa ni Lungula Pina( 35) na Agustino  Pascal( 60) wote wakazi wa Kijiji cha Kapanga Tarafa ya Mwese Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi 
Alisema watuhumiwa  walikamatwa  kijijini hapo mnamo Agosti 1 mwaka huu majira ya saa tisa  na nusu alasiri  wakiwa  na madawa hayo ya kulevya  aina ya Bangi gunia tatu na mbegu zake kilo mbili
Kidavashari alieleza watuhumiwa walikamatwa kufuatia taarifa  za  zilizokuwa zimelifikia jeshi la polisi kuwa  watuhumiwa hao wanajishughulisha   na biashara ya kuuza na kusambaza  Bangi na kulima  Bangi 
Alisema  mtuhumiwa Lungula Pina  yeye kabla ya kukamatwa siku hiyo alikuwa akituhumiwa  kujihusisha na kulangua Bangi na kuisambaza katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi na Mikoa ya jirani 
Na Mtuhuhumiwa Agustino  yeye amekuwa akijishughulisha na kilimo  hicho  cha Bangi kwa muda mrefu sasa   na  amekuwa ni miongoni mwa wakulima maarufu kijijini hapo wa  madawa hayo ya kulevya 
Kidavashari alisema mbali ya kukamata Bangi hiyo  na mbegu zake jeshi la polisi liliweza kuteketeza  kwa moto Bangi  za  watuhumiwa  zaidi ya eka moja ambayo ilikuwa bado ipo shambani ambayo ilikuwa bado haija vunwa 
Alisema  jeshi la polisi Mkoa wa Katavi lanaendelea na msako usio  na kikomo  ili kuwabaini watu wengine ambao wanajishughulisha  na kilimo na kuuza   madawa ya kulevya  Katika wilaya zate za Mkoa huu
Na Walter Mguluchuma,Mpanda


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo