AMUUA MKEWE NA KUMNING'INIZA JUU YA MTI

POLISI  mkoani Katavi  inamshikilia mkazi wa  kijiji  cha Itetemya, Tarafa ya Karema   wilayani  Mpanda , Masanja  Kulwa (23)   akituhumiwa kumuua  mkewe  wa ndoa Nyingi Shida (21)  kwa  kumnyonga  kisha  kumfunga na  kipande cha chandarua  na  kumning'iniza mtini.
 
Inadaiwa chanzo  cha  mauaji  hayo  ni  wivu  wa kimapenzi  ambapo  mke  alikuwa akimtuhumu  mumewe mara kwa  mara kuwa  alikuwa na mahusiano   ya kimapenzi   na  mwanamke  mwingine  kijijijini  humo 
 
Kwa mujibu  wa Kamanda wa Polisi mkoni Katavi  Dhahiri kidavashari    mumewe wa marehemu  huyo  inadaiwa  alimfanyia ukatili  huo  mkewe  huu  baada ya kuchukizwa  na  kitendo  cha mkewe  huyo  kwenda kumfokea  mwanamke ambaye inadaiwa  kuwa   ni ‘ mpenzi ‘ wake.
 
Kamanda Kidavashari  aliongeza kuwa  mtuhumiwa  baada  ya  kuvunja shingo la mkewe   alimfunga  na kipande cha  chandarua   chandarua  shingoni  mwake na kumning’iniza   mtini  mita  70  kutoka  nyumbani  kwao .
 
Aliongeza kuwa   tukio hilo  lilitokea  Julai 31 , mwaka huu  saa  sita usiku  kijijini  humo  baada ya  wanandoa  hao  kuzozana na kushutumia  ambapo  marehemu anadaiwa  kukasirishwa  na  tabia  ya  mumewe kuwa na mahusiano  na  mwanamke  kijijini  humo..
 
 Kidavashari  alidai kuwa siku  moja  kabla ya tukio hilo  kutokea  marehemu  akiwa   amejifunga ‘kibwebe”  alikwenda nyumba kwa  mwanamke  mwezake kijijini  humo  usiku   na kumwonya  aache    kuwa na   mahusiano  ya  kimapenzi  na mumewe .‘.
 
Inadaiwa  ndipo  wanandoa  hao  waliposhindwa kuelelewana  na  kuanza kupigana  ambapo  alfajiri ya  siku  iliyofuata  wapiti njia  waliuona mwili wa marehemu  ukiwa unaning’inia  mtini  akiwa  ameshakufa ambapo  mara moja  walimsaka  mshutumiwa  na kumkamata  kisha kumkabidhi  katika  Kituo  cha Polisi  .
 
Kwa mujibu  kidavashari  uchunguzi  wa  kitabibu  alibainisha kuwa  shingo  la  marehemu huyo  lilikuwa limevunjika  huku  akiwa  na  majeraha  yaliyotokana  na kipigo  katika  sehemu  mbalimbali za mwili  wake  ambapo  alionekana  kuwa  na majeraha  makubwa  mdomoni .
 
Kamanda Kidavashari  amedai  kuwa  mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa  mahakamani   wakati wowote  mara tu  baada  ya  uchunguzi  wa awali  wa  shauri  hilo  la mauaji  kukamilika 
 
na walter mguluchuma mpanda katavi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo