Watu wasiojulikana wamevunja transfoma ya umeme na kuiba mafuta na
waya za kopa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milion 70 katika mradi
wa kusambaza umeme unaofanywa na kampuni ya Symbion katika kata ya
Tubuyu na Tungi katika manispaa ya Morogoro.
Mwakilishi wa kampuni ya Symbioni akizungumza katika tukio hilo
amesema hiyo sio mara ya kwanza kutokea na kuwa vitendo vya kuhujumu
miundombinu ya umeme inakwamisha kukamilika kwa shughuli za kusambaza
umeme kwa wananchi na kutaka jeshi la polisi kusaidia ili kupatikana kwa
waliohusika.
Nao wananchi katika eneo la tubuyu wamelalamikia kitendo hicho huku
wakitupia lawama huenda hujuma hiyo imefanywa na wataalamu wenye ujuzi
na fani ya umeme huku wakiomba msaada wa vyombo vya sheria kuweza
kuwatia hatia waliohusika kwani hujuma hizo zinasababisha kusimama kwa
mradi wa kusambaza umeme kwa wananchi.
na itv