Wakazi wa Mabibo External jijini Dar es Salaam wamekusanyika nje ya
lango kuu la kuingia katika kanisa la Victorious Living lilipo katika
eneo hilo kuushinikiza uongozi wa kanisa kuweka vifaa maaalum vya
kuzuia kelele wakati wanapofanya ibada zao.
Wakazi wa Tabata External wamekusanyika nje ya lango kuu la kuingia
katika kanisa la Victory Living lilipo katika eneo hilo kushinikiza
uongozi wa kanisa kuweka vifaa maaalum vya kuzuia kelele wakati
wanapofanya ibada zao kutokana na kanisa hilo kutumia vyombo vyenye
sauti kubwa ilihali kanisa hilo lipo katika makazi ya watu.
Wakizungumza nje la kanisa hilo waumini hao wamesema hawana shinda
na huduma zinazotolewa na kanisa hilo bali ni namna ambavyo wanafungulia
vyombo vya muziki kwa sauti ya juu na hivyo wanajikuta usiku mzima
hawalali hasa wagonjwa.
Baadhi ya wakina mama wanaoishi jirani na kanisa hilo wamesema
watoto wao sasa wameanza kuonesha hali ya utofauti kutokana na ukweli
kuwa usiku hawalali na mchana hawalali kutokana na makelele hayo na
hivyo wanaziomba mamlaka husika zione nini cha kufanya.
Akijibu tuhuma hizo mchungaji kiongozi wa kanisa hilo mchungaji
John Saidi amekiri kuwepo na malalamiko ya siku nyingine kati yake na
wananchi wa eneo hilo lakini amekuwa akijitahidi mara kwa mara kupata
ufumbuzi wa kero hizo ikiwemo kufuta baadhi ya huduma zinazotolewa
kanisa lake, huku afisa mtendaji wa mtaa huo Bw Henry Mtogo akikiri
kupokea malamamiko ya wananchi hao.
CHANZO:ITV