Ifuatayo ni habari moja yenye muunganisho wa taarifa mbili
kumhusu Sheikh Ponda. Awali ni taarifa ya yaliyotukia Morogoro hapo jana
na inayofuata ni habari ya juzi kuhusu agizo la DPP la kutaka akamatwe.
John Nditi via Globu ya Jamii, Morogoro —
KATIBU wa Jumuiya ya Kiislamu nchini , Shekhe Ponda Issa Ponda,
alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuumizwa na kitu kinachodhaniwa
kuwa ni risasi kwenye bega lake la kulia wakati akiekelea katika Msikiti
wa Mungu Mmoja Dini Moja wa Mjini Morogoro baada ya kumalizika kwa
kongamano ya Dini ya Kiislamu.
Mkasa huyo ulitokea Jumamosi
Augosti 10, mwaka huu majira ya saa 12:15 za jioni eneo la barabara ya
Tumbaku karibu na Fire, mara baada ya kumaliza kwa Kongamano la Kiislamu
lililofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege, Kata
ya Saba Saba, Manispaa ya Morogoro.
Shekhe Ponda alishiriki
katika Kongamano hilo lililoandaliwa na Umoja wa Wahadhiri wa Dini ya
Kiislamu Mkoani Morogoro na kufanyika siku ya Idd Pili kuanza saa nane
mchana hadi kumi na mbili jioni ya siku hiyo.
Kongamano hilo
lilipata baraka zote na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, ambalo lilitoa
masharti kadhaa ya kuzingatiwa na wazungumzaji ikiwa ni kutokashifu
dini nyingine wala viongozi wa serikali.
Sakata la kutaka
kutiwa mbaroni kwa Shekhe Ponda lilikuja baada ya yeye kudaiwa kukiuka
masharti ya Mahakama aliyopewa baada ya kuhukumiwa kifungo cha mwaka
mmoja nje wa kutakiwa asitende kosa lolote la jinai anapotumikia adhabu
hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadalizi ya Kongamano hilo, Ustaadhi Idd Msema, alidai kuwa Shekhe Ponda
baada ya kutoka ndani ya
gari eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege aliofika mita
chache katika barabara ya Tumbaku alitelemka na wakat akitaka kuingia
garini ilifayuliwa risasi iliyompiga begani.
Ustaadh
Msema alidai kuwa baada ya kupigwa risasi begani waumini waliokuwa
wameambatana naye walimchukua na kumpakiza kwenye Pikipiki hadi
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili kupoatiwa matibabu.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti huyo, baada ya kufika hospitali, waliona
anacheleweshwa kpatiwa matibabu na ndipo walipoamua kumwondoa na
kumpekea kwenye Hospitali binafsi ambayo hakupenda kuitaja.
Akizungumzia
kwa kina hali ya Shekhe Ponda baada ya kujeruhiwa huko, alisema kuwa yu
hai licha ya kuumia vibaya begani na kwamba wanatarajia kumpekela eneo
jingine hususani Jijini Dar es Salaam kupata matibabu zaidi.
Alisema
viongozi wa Umoja huo hauwezi kuweka wazi sehemu anakotibiwa kwa kuwa
jambo hilo ni la kiusalama zaidi hasa wakati huu ambapo kumekuwa na
sinto fahamu.
Baadhi ya walinzi wa
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro waliozungumza juu ya tukio hilo ,
walikiri kuwa Shekhe Ponda aliletwa hapo kwa usafiri wa Piki piki
zikiambatana na nyingine zaidi ya 50 na kuishia getini.
Walisema
walimwingiza adi mapokezi na kwamba walipoona umati mkubwa upo getini
waliamua kutoa taarifa Polisi kuwa wamevamiwa na watu ambapo muda si
mrefu Polisi wa FFU waliwasili na gari lao Hospitalini hapo.
Hata
hivyo walinzi hao walisema, baada ya kuona Askari wamefika Hospitalini
hapo, baadhi ya wafuasi wa Shekhe Ponda waliamua kumyanyua na kumbeba
mabegani na kutoka naye mlango mwingine wakimlazimisha mlinzi
kuwafungulia mlango na baadaye wakatokomea naye kwa usafiri wa Pikipiki
kusikojulikana.
Kufikishwa kwa Sheshe
Ponda katika Hosipitali ya Rufaa kulithibishiwa pia na Mwenyekiti huyo
ambaye alidai kuwa waliamua kumwondoa baada ya kuchekewa kupatiwa
huduma.
Baada ya tukio hilo, uvumi
ulisambaa meneo mbalimbali nchini ukidai kuwa Shekhe Ponda amepigwa
risasi na Polisi na kufariki dunia. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Morogoro, Feustine Shilongine akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi
majira ya saa tatu usiku wa Augosti 10, baada ya kutokea kwa tukio hilo,
alisema kuwa hapakuwa na taarifa juu ya kutokea kifo cha Shekhe Ponda.
“
Nimepingiwa simu zaidi ya 50 , zikiulizia jambo hili...kuwa Ponda
amefariki dunia ...Binafasi nami ninazisikia , ujumbe umesambazwa kwenye
simu za watu mbalimbali...tumezunguka kila mahali hakuna kifo wala
maiti yake ...na vijana wangu wanaendelea kulifuatilia suala hili”
alisema Kamanda huyo.
Juhudi za
kufuatilia sakata la uvumi kifo cha Shekhe Ponda uliendelea kufanyiwa
kazi na Ripota a wetu huyu na usiku wa saaa tano Mwenyekiti wa Kamati
huyo aliweka wazi kwa kusema kuwa Shekhe Ponda yu hai isipokuwa ameumia
vibaya sehemu ya bega .
“ Nipo katika
eneo ambalo Shekhe Ponda anapatiwa matibabu...sehemu ambayo hatuwezi
kupataja kiusalama , isipo kuwa ameumia vibaya kwenye bega lake. Lakini
yu hai wala hajafa” alisema Msema.
Polisi Mkoani hapa bado haijatoa taarifa rasmi kuhusiana na sakata hilo, nasi twaendelea kufuatulia kwa ukaribu.
--- MWISHO wa Taarifa kutoka kwa John Nditi---
Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/08/taarifa-ya-kilichojiri-morogoro-kuhusu-sheikh-ponda.html#ixzz2beGMqkLr
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi