Katika mitandao hivi karibuni zilionekana picha za watanzania wawili waliovamiwa na kupigwa vibaya Ugiriki.
Picha hizo hazikuwa na maelezo ya kutosha na hatimae zilizusha maswali mengi yaliyokosa majibu muwafaka.
Jumuiya ya watanzania ugiriki baada ya kikao cha tume maalum inapenda kutoa taarifa kamili ifuatayo:
1. Waliovamiwa
ni Makamu Mwenyekiti bw. SALUM MSELEM na Mhazina bw. SAID MOHAMED
SAID maarufu kwa jina la NURAMO(CHIDI) NDUGU HAWA SI WAKIMBIZI, NI
WATANZANIA HALISI.
2. Mabwana hao walikuwa wanapita kwenye
garden usiku wa Jumatano 01/08/2013 kuelekea makwao,wakitokea kwenye
kikao muhimu ofisini . Karibu na garden hiyo kulikuwa na wezi
waliokuwa wanajaribu kuvunja gari iliyokuwa imeegeshwa.Wezi hao
walijishuku kama Salum kawagundua wakamfuata kwa vitisho na kuanza
kumpiga.
Wakati huo lilitokea kundi lao jingine la watu wasiopungua
kumi wakaanza kumkimbiza Chidi ambaye alijitahidi kukimbia hadi kufika
chini ya nyumba anayoishi Salum(umbali wa mita 50) huku akipiga kelele
na hapo waliendelea kumpiga.Kelele za Chidi kwa bahati zilisikika na mke
wa Salum ambae nae alipiga kelele za kuomba msaada zilizowafanya
wakimbie na kumwacha Chidi akiwa hoi.
3. Ndugu zetu
tuliwafikisha hospitali na tulitoa ripoti polisi wanaoendelea na
uchunguzi ambao hadi wakati huu tunapoandika maelezo haya HAKUNA TAARIFA
ZOZOTE CHANYA ZA KUWAKAMATA WAHUSIKA.
4. Uongozi wa jumuiya
unashindwa kutamka kuwa wezi hawa wana uhusiano na kile kikundi maarufu
kinachochukia na kuwavamia wageni.Hatuna ushahidi.Bali tuna imani
kubwa walikuwa ni vibaka toka nchi jirani.
5. Tumeamua kuutaarifu ubalozi na vyombo vyote vya habari vilivyokuwa vimetumiwa taarifa za awali za tukio hili.
6. Mwisho jumuiya yetu inatangaza bila kusita:
VIONGOZI WETU HAWAKUFANYA BAYA LOLOTE LILILOSABABISHA WAVAMIWE NA KUPIGWA. TUPO PAMOJA NAO KWA HALI NA MALI.
Ahsanteni
Ahsanteni
Kny
TUME MAALUM YA JUMUIYA.
(Kayu Ligopora)
Source: Michuzi
TUME MAALUM YA JUMUIYA.
(Kayu Ligopora)
Source: Michuzi