Rais Uhuru Kenyatta akutana na Rais Mstaafu Daniel arap Moi ikulu,
Nairobi Agosti 1, 2013. Walishauriana kuhusu mikakati ya kudumisha amani
Afrika Mashariki na eneo la Maziwa Makuu. Picha/PSCU
=======
RAIS Uhuru Kenyatta Alhamisi Hii alikutana na kushauriana na Rais Mstaafu Daniel arap Moi ikulu, Nairobi. Wawili hao walishauriana kuhusu mikakati ya kudumisha amani Afrika Mashariki na eneo la Maziwa Makuu.
Mkutano wao ulijiri siku moja tu
baada ya viongozi wa Afrika Mashariki na Maziwa Makuu kukutana Gigiri,
Nairobi kwa Kongamano la Kimataifa Kuhusu eneo la Maziwa Makuu (ICGLR).
Mkutano huo ulijadili mizozo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan.
Baada ya mkutano huo, viongozi
hao waliunga mkono mashauriano kati ya serikali ya DR Congo na waasi wa
M23 yaliyofanikishwa na Uganda na kutaka pande zote ziendelee na
mashauriano hayo.
Pia walizitaka Uganda na Sudan Kusini ziendelee kuheshimu makubaliano ya kudumisha amani.
Waliohudhuria kongamano hilo ni
pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Rais Yoweri Museveni wa Uganda
na Rais Michel A.M. Nondokro Djotodia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.