Kisiwa cha Migingo.
Waliwapokonya wavuvi hao kilo 1,000 za samaki wa thamani ya Sh200,000 katika ufuo wa Mugabo kaunti ya Migori Jumanne jioni.
Raia wa Uganda walidai kuwa wavuvi hao walikuwa wameingia katika sehemu yao ya ziwa bila ruhusa.
Maafisa hao
waliokuwa wamejihami waliwazuilia wavuvi hao waliokuwa bado ndani ya
ziwa na kuwapokonya samaki hao huku wakiwatishia kwa bunduki.
Mkuu wa
Wilaya ya Nyatike Moses Ivuto alisema Maafisa wa serikali ya Kenya
watakutana na wenzao wa Uganda ili kujadiliana kuhusu mzozo huo wa
uvuvi.
“Tutaenda kujadiliana kuhusu suluhu ya mizozo ambayo imeendelea kuhusisha ziwa hili,” alisema.
Wavuvi wa Kenya walidai kuwa samaki wanaopokonywa huuziwa bwenyenye mmoja kutoka Uganda.
Wiki moja iliyopita, maafisa wa Uganda walitoroka na tani mbili za samaki yenye thamani ya Sh500,000 kutoka kwa wavuvi wa Kenya.
Maafisa hao ambao wamekita kambi katika kisiwa tata cha Migingo waliwapokonya wavuvi hao samaki huku wakiwatisha kwa bunduki.
Mwenyekiti wa
Usimamizi wa Uvuvi katika kisiwa cha Migingo Juma Ombori alisema
maafisa hao waliojihami waliwavamia wavuvi hao wakati walikuwa wanarejea
kuvua samaki majira ya usiku.
Gavana wa kaunti ya Migori Okoth Obado alitoa wito kwa serikali ya Uganda kuheshimu Wakenya.
Alisema
RaisYoweri Museveni anapaswa kuwaondoa maafisa wake wa usalama kutoka
kisima hicho kama njia ya kudumisha ujirani mwema na Kenya.
“Nimeongea na
Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kuhusu mzozo wa Migingo
na wote wawili wamenihakikishia kuwa serikali inashughulikia jambo hilo
kwa haraka,” Bw Obado aliwaambia waandishi wa habari.
Mzozo wa kisiwa cha Migingo ulianza 2009 nchi zote mbili zikingangania kukimiliki.