
Taarifa kutoka Ikulu ilisema hatua hiyo imechukuliwa ili kulainisha mawasiliano kutoka kwa serikali.
“Ofisi ya Katibu wa Mawasiliano
ya Umma na Msemaji wa Serikali haiingiani na muundo mpya wa utawala wa
Rais Uhuru Kenyatta na imevunjwa,” ilisema taarifa ya PSCU.
Msemaji wa Ikulu Manoah Esipisu atatekeleza majukumu yaliyokuwa yakitekelezwa na msemaji wa serikali kwa mujibu wa taarifa hiyo.
Dkt Alfred Mutua alikuwa wa
kwanza kuhudumu katika wadhifa huo na akarithiwa na Bw Kariuki. Bw
Kariuki aliteuliwa na Rais Mstaafu Kibaki kabla ya kustaafu kwake.
Dkt Mutua kwa sasa ndiye gavana wa Kaunti ya Machakos.