Akionesha Jeraha alilopata baada ya kipigo.
Jeshi la polisi mkoani ruvuma limeingia lawamani baada ya askari wake
kudaiwa kumshambulia, Bwana Omary Hamis mkazi wa Mfaranyaki Makaburini
na kumvunja mara mbili mkono wa kulia na bega la kushoto na kumjeruhi
maeneo mbalimbali ya mwili wake baada ya kupigana na mkewe ambapo
amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma kwa matibabu.
Askari wa jeshi hilo wanadaiwa kumshambulia bw.
Omary Hamis mkazi wa Mfaranyaki Songea huku watoto wake wakishuhudia na
kumpiga kwa virungu na kumvunja mkono wa kulia na bega la kushoto na
kumsababishia majeraha mbambali kwenye mwili wake baada ya mwananchi
huyo kupigana na mkewe aliyewapigia simu polisi kutokana ugomvi
waliokuwa nao mke na mume.
Mtoto wa bw. Abubakary Omary mwenye miaka 11 alishudia tukio hilo wakati baba yake ikipata kipigo hicho.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma bw.
George Chiposi alipofuatwa ofisini kwake kwa siku mbili mfululizo
aweze kuzungumzia tukio hilo hakuweza kupatikana na alipotafutwa kwa
simu yake ya mkononi na kuelezwa kuhusiana na tukio hilo hakusema
chohote na kukata simu.
NA Joseph Mwambije, Songea