skip to main |
skip to sidebar
KAGAME ASHAURIWA KUSIKILIZA USHAURI WA KIKWETE
Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dk. Richard Sezibera, ametoa
kauli ya kumtaka Rais wa Rwanda, Paul Kagame kutumia busara kwa
kusikiliza ushauri wa kidiplomasia aliopewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete kwa sababu ushauri huo
umezingatia maslahi ya nchi ya Rwanda na wananchi wake kwa ujumla.
Dr. Richard Sezibera alisema inampasa Rais Kagame aache kutoa maneno ya
kashfa dhidi ya Rais Kikwete na asichukulie kwa kuwa Rais Kikwete yuko
kimya basi inamaanisha amekubaliana na kashfa zake na za wanyarwanda,
isipokuwa Rais Kikwete anatumia busara ambayo ni muhimu sana kwa usalama
wa ukanda huu wa Afrika.
Aliendelea kuisifu Tanzania kwani pamoja na dhihaka inayotolewa na Rais
Kagame dhidi ya Rais Kikwete, hakuna lolote mbaya ambalo Tanzania
imelifanya kuathiri utendaji kazi wa wafanyakazi wa ofisi za Makao Makuu
ya Jumuiya jijini Arusha. Wanyarwanda waliopo hapa wanaendelea na kazi
zao bila kubughudhiwa jambo ambalo linaonyesha uungwana wa Tanzania.
Dr. Richard Sezibera aliyasema hayo jijini Arusha alipokuwa anaongea na
waandishi wa habari kuhusu uendeshaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi