NG'OMBE 80 WAUAWA KWA KUKATWA MAPANGA


 dead-cows_1210641i

Ng’ombe zaidi ya 80 wameuawa kikatili kwa kukatwakatwa mapanga na wengine kuchinjwa baada ya kuingia katika mashamba ya wakulima wa Vijiji vya Kisara na Mbogo, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
 
Tukio hilo ambalo liliamsha hasira kwa wamiliki wa ng’ombe hao lilitokea Agosti 19 katika vijiji hivyo maeneo ya mashambani na kwamba tukio hilo limefanywa na watu wasiojulikana ambao wanadhaniwa kuwa ni wakulima wenye mashamba katika vijiji hivyo.
Ng’ombe wengine walikuwa wamevunjwa miguu na hivyo kushindwa kutembea ambapo wamiliki wa ng’ombe hao waliwashutumu wakulima kwa kuchukua sheria mkononi na hivyo kuiomba Serikali kuchukua hatua zinazostahiki ikiwa ni pamoja kuwasaka waliohusika katika tukio hilo.
Nao baadhi ya wakulima wilayani humo walionyeshwa kusikitishwa na tukio hilo .huku wakiiomba Serikali kuhakikisha inapanga mipango mizuri ili kunusuru migogoro ya wakulima na wafuagaji ambayo inaweza kusababisha machafuko kwenye vijiji.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alisema kuwa Serikali ya Wilaya imeanza kuchukua hatua kwa kushirikiana na polisi ili waliohusika katika tukio hilo waweze kuwakamata na kuchukuliwa hatua za kisheria.

CHANZO:MWANANCHI


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo