MWANAMKE ACHAPWA VIBOKO ARUSHA KWA KUVAA NGUO FUPI

Msichana mmoja ambaye jina lake halikujulika amejikukuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na   kuchapwa viboko na kundi la watu katika eneo la soko la NMC jiji Arusha kwa madai ya kuvaa nguo fupi hali iliyowalazimu wasamaria wema kuingilia kati  na kutumia nguvu kubwa ili  kumwokoa na kumsitiri kwa kumfunika na nguo zingine.

Mwandishi wetu Halfani Lihundi  kutoka Arusha alikuwapo katika sakata hilo na ametuma taarifa hii iliyosema,  watu walio shuhudia tukio hilo wamesema wamechukizwa na aina ya nguo alizizovaa msichana huyo ambazo haziendani na maadili ya Kitanzania, ndiyo maana wameamua kumwadabisha ili kukomesha tabia hiyo.

Kwa upande wao wanawake waliyo msitiri msichana huyo kwa kumpa nguo za heshima na kumhifadhi katika Gareji ya jirani kabla ya kumkimbiza kwa gari aina ya Toyota Hiace wamesema hawaridhishwi na tabia hiyo inayowadhalilisha wanawake na kuwataka wasichana kuavaa nguo za kujisitiri ili kujenga heshima katika jamii.
 
na itv


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo