JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia kijana mwenye umri wa
miaka 15 mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari
Kelamfua iliyopo wilayani Rombo baada ya kukutwa akimwingilia ndama wa
ng'ombe.
Akithibitisha, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz
alisema tukio hilo lilitokea Agosti 3 mwaka huu saa 5:10 usiku nyumbani
kwao Kelamfua.
Boaz alisema kuwa baba wa kijana huyo ndiye aliyemfumania kwa kuwa
alikuwa akimfuatilia kwa muda mrefu na ndipo alipomkamata.
Alisema kuwa kabla ya tukio hilo kijana huyo aliwahi kukutwa akifanya
mapenzi na kuku na kuanzia hapo mzazi wake huyo akaanza kumfuatilia na
hivyo kumkamata akifanya mapenzi na ng'ombe ambaye ni ndama.
Kamanda alisema kuwa baada ya kukamatwa kijana huyo alifikishwa kituo
cha polisi na kuhojiwa ambapo alikiri kufanya kitendo hicho na kueleza
kuwa amekuwa akitafuta wasichana bila mafanikio.
Aidha aliongeza kuwa kila msichana anayemtamkia neno la mapenzi amekuwa
akitaka fedha nyingi wakati yeye ni mwanafunzi hana uwezo wa kupata fedha.
Boaz alisema kuwa baba wa kijana huyo alishapata taarifa siku za nyuma
kuhusiana na tabia ya kijana wake huyo na ndipo akaanza kumfuatilia na
kwa sasa anashikiliwa na polisi uchunguzi zaidi ukiendelea.
chanzo:habarileo
