MTANGAZAJI WA TBC FM ATANGAZA KUWASAKA WEZI WALIOIBA VITU NDANI YA GARI LAKE!!!


 D'JARO ARUNGU Mtangazaji nguli wa TBC FM
Gari la mtangazaji huyu likipigwa mng'ao siku hiyo ya tukio baada ya kutengenezwa.
Ujumbe alioandika baada ya
tukio
YULE mtangazaji maarufu hapa nchini ambaye pia ni mmiliki wa Website ya http://www.babamzazi.com/ alieibiwa Radio na baadhi ya vitu ndani ya gari lake katika pub moja inayotambulika kwa jina la KBC Pub ilioko njia panda ya Uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere Jijini Dar Es Salaam sasa atoa tamko kwamba kutokana na tetesi kwamba vidokozi waliodokoa vitu hivyo katika gari lake sasa anawasaka kimya kimya na akiwakamata Sheria itafuata mkondo wake,.
 
Tukio hili ni tukio la aina yake lilitokea takribani mwezi sasa, D'JARO ARUNGU aliondoka nyumbani kwake kwa hasira baada ya kukwaruzana na mkewe nyumba kwake anakoishi huko maeneo ya Mombasa Gongo la mboto na kuamua kwenda kupata moja moto moja baridi huko Njia panda ya uwanja wa ndege katika Pub hio (KBC PUB) Majira ya saa nne kasoro usiku Kama kawaida alikutana na marafiki wakaendelea kubadilishana mawazo ya hapa na pale kupoteza mawazo ya hasira alizopewa na shemejiyetu. mara akashangaa kumepambazuka! Si unajua tena mambo ya stori yalivyo hasa mnapokutana watu zaidi ya wawili?.. 
 
Basi baada ya kutoka nje na kufungua mlango wa gari D'JARO alitaharuki kuona nyaya zinaning'inia kwenye dashbord ya gari, Radio ya gari hakuna nguo za mazoezi aliacha kwenye gari hazipo na kibaya zaidi alipojaribu kuwasha gari halikuwaka liliishia kupiga king'ora (Alarm). 
 
Ilimbidi amtafute fundi akarekebisha gari likawa sawa.Hapo nipo alipoandika ujumbe mfupi kwenye simu yake ya kiganjani kama mnavyouona hapo juu, Na kuamua kuelekea kazini kwake TBC Fm kulisongesha.
 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo