MGANGA mmoja wa
kienyeji aliyefahamika kwa jina la George Tereva (55) amefariki dunia
baada ya kupigwa risasi maeneo ya tumboni,kichwani na kwenye paji la uso
kisha kukaktwa na panga kichwani na watu wawili wasiojulikana.
Akithibitisha kutokea
kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi (Pichani) alisema kuwa
tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa moja na nusu katika kijiji cha Lungemba
kata ya Lungemba wilaya ya Mufindi.
Kamanda alisema kuwa
watuhumiwa wa tukio hilo wanatafutwa na jeshi la polisi na mara
watakapopatikana watafikishwa Mahakamani uchunguzi utakapo kamilika.
Kamanda alibainisha kuwa
chanzo cha tukio hilo hakijajulikana
CHANZO:JIACHIE